Na Antony Sollo - MWANZA.
KAMPUNI ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC)inayojenga daraja la JPM imelipongeza Jeshi la Polisi kwa kufanikisha kukamata mali zake zilizokuwa zimeibiwa katika ujenzi wa Mradi wa Kimkakati wa daraja la Dkt. John Pombe Magufuli linalojengwa katika kivuko cha Kigongo-Busisi Jijini Mwanza.
Kufuatia Kampuni hiyo kuripoti tukio la wizi katika Kituo cha Polisi Jijini Mwanza Askari wa Jeshi la Polisi walianza msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa hao Jeshi la Polisi lilipata taarifa za kiintelijensia ambazo ziliwasaidia Askari hao kufika katika kitongoji cha Busisi madukani kwenye nyumba inayomilikiwa na Makona Samwel na kufanikiwa kupata vitu mbalimbali vikiwa vimefichwa ndani ya nyumba hiyo.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP) Wilbroad Mutafungwa alisema kuwa baada Askari hao kufanya upekuzi katika chumba cha mfanyakazi wa kampuni ya CCECC Halfani Seif@Yusuph walifanikiwa kuvikuta vifaa vyote vilivyoibiwa katika mradi wa kimkakati wa daraja la JPM.
“katika chumba ambacho anaishi Halfan Seif mfanyakazi wa CCECC ambaye ni fundi nondo ( Stell fixture)anayedaiwa kushirikiana na walinzi kufanikisha wizi huo tulifanikiwa kukuta vitu vyote vilivyokuwa vimeibiwa na uchunguzi utakapokamilika watuhumiwa hao watafikishwa Mahakamani kwa hatua Zaidi”alisema Kamanda Mutafungwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi vitu vilivyokamatwa ni pamoja na Mashine Saba za kuchomelea,Stick za kuchomelea vyuma aina ya THJ 422 Box 30, Welding Cable na Drilling Bit mbili ambapo thamani yake bado haijahamika mara moja.
Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa mtuhumiwa huyo alishirikiana na Hamfrey William ambaye pia ni mfanyakazi wa kampuni ya CCECC kama fundi wa kuchomelea pamoja na mlinzi wa kampuni ya ulinzi COPS SECURITY TANZANIA LIMITED aliyejulikana kwa jina la Bwire Musiba Manyama(30)ambao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya upelelezi zaidi.
Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linashikilia gari aina ya Toyota NOAH rangi nyeusi yenye namba za usajili wa namba T 707 BPG inayosadikiwa kuhusika katika kubeba vitu vilivyoibwa baada ya kukutwa limetelekezwa eneo la Busisi madukani Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza.
Kwa upande wake (HR) wa Kampuni ya CCECC Denise Peter na Yang Neng wamelipongeza Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kwa kufanikisha ukamataji wa vitu hivyo vilivyoibwa na kuomba kuliomba Jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi katika maeneo ya Mradi huo.
Kamanda Mutafungwa amewataka wananchi kuendelea kushilikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili ziwezekufanyiwa kazi kwa wakati na Mkoa wetu kuendelea kuwa shwari.

Chapisha Maoni