Top News

Wananchi Isaka:tunamshukuru Ras Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza Miradi ya kimkakati.

 

 Wananchi Isaka:tunamshukuru Ras Dkt  Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza Miradi yakimkakati.

 Na Antony Sollo - SHINYANGA.

WANANCHI wakazi wa Kijiji cha Isaka,kata ya Isaka Mkoani Shinyanga wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa hatua zake kuendeleza Miradi ya kimkakakati iliyoasisiwa na Mtangulizi wake Hayati Dkt John Pombe Magufuli.

Wananchi hao wameyasema hayo wakati wa ziara ya waandishi wa Habari waliotembelea Mradi wa ujenzi wa Reli ya mwendo kasi SGR ili kujionea mambo mbalimbali ikiwemo maendeleo ya Mradi unaojengwa katika kipande cha Mwanza hadi Isaka chenye urefu wa Km 341 ikiwa ni km 249 njia kuu na km 92 njia za kupishania.

Aizungumza na waaandishi wa Habari,Mwenyekiti wa Kijiji cha Isaka Shaban Jumanne Khamis ambaye pia ni mmoja wa wananchi waliopisha Mradi wa SGR alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt  Samia Suluhu Hassan huku akitaja mafanikio lukuki waliyopata kutokana na Mradi huo.

“Kiuhalisia namshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt  Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza Miradi mbalimbali ya kimkakati iliyoasisiwa na mtangulizi wake Hayati Dkt John Pombe Magufuli yapo mambo mengi yanasemwa Mtandaoni lakini kiukweli mtu yeyote anapofanya jambo zuri hakosi watu wa kumpinga,sisi wananchi wa Isaka tuko pamoja na Rais katika uungaji mkono ujenzi wa Taifa letu”alisema Mwenyekiti huyo.

Mwenyekiti huyo ameyataja manufaa mengi yanayotokana na Mradi huo kuwa ni pamoja na kurahisisha usafiri,kupata Makazi bora baada ya kulipwa fidia,kununua vifaa vya kulimia Power tiller (nyenzo za kilimo),kusomesha watoto Shule,pamoja na ununuzi wa chakula na kuinuka kiuchumi kwa ujumla wake.

Kwa upande wake,Meneja Mradi Christopher Kalist aliwashukuru wananchi wa Kijiji cha Isaka kwa kuitikia wito wa Serikali wa kupisha Mradi uliopita katika maeneo yao kwa hiari kupisha ujenzi wa reli hiyo ambayo baada ya kukamilika itakuza Uchumi wa wananchi na pamoja na pato la Taifa kwa ujumla.

“kipekee kabisa napenda kumshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumpatia fedha Mkandarasi anayejenga Reli hiyo ili kuweza kuikamilisha kwa muda uliopangwa kwa mujibu wa mkataba lakini pia niwapongeze sana wananchi wa maeneo mbalimbali ambao maeneo yao yamepitiwa na Mradi huu wa SGR sisi kabla ya kutwaa maeneo hayo tulichukua hatua ya kukutana nao na kuwapa Elimu kuhusu faida za Mradi huu,walielewa na ndiyo maana hakuna malalamiko wala mgogoro wowote katika Mradi huu”alisema Mhandisi Kalist.

Mhandisi Christopher alisema kuwa katika Mradi huo kutakuwa na Vituo/Stesheni kumi (10) kwa ajili ya kupakia na kushusha Abiria na kuzitaja kuwa ni Isaka,Luhumbo,Shinyanga,Seke,Malampaka,Malya,Mantare,Bukwimba,Fela na Mwanza huku akiwataka watanzania kujitokeza na kuunga mkono juhudi za Serikali za kujenga uchumi kwa kuchangamkia fursa zilizopo katika maeneo yao kutokana na ujenzi wa Mradi wa SGR. 

Kwa mujibu wa Mhandisi Christopher Kalist,mpaka sasa Serikali imeweza kuokoa fedha nyingi kutokana na kumshauri Mkandarasi kujenga Kiwanda cha kutengeneza Mataruma kilichojengwa katika Kijiji cha Seke Kata ya Seke Bugoro Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga ambacho kimetoa fursa ya ajira kwa vijana 200 kama Ilani ya Chama cha Mapinduzi inavyoelekeza

Imeelezwa kuwa bila umakini wa wataalamu kuishauri  Serikali kwenye utakelezaji wa Mradi huo kujenga Kiwanda cha kutengeneza Mataruma ndani ya nchi na iwapo mataruma hayo yangeagizwa nje ya nchi gharama zingekuwa kubwa Zaidi kwa kuwa inakadiriwa taruma moja linagharimu fedha za kitanzania zaidi ya Sh 400,000 kwa taruma moja na likitengenezwa nchini gharama zinakuwa ni Sh 400,000 pekee huku ikielezwa kuwa baada ya Mradi kukamilika kiwanda hicho kitabaki kuwa ni mali ya Serikali.

“bila umakini wa wataalamu kuishauri vizuri Serikali na iwapo mataruma hayo yangeagizwa nje ya nchi gharama zingekuwa kubwa zaidi kwa kuwa inakadiriwa kuwa taruma moja linagharimu fedha za kitanzania zaidi ya Sh 400,000 kwa taruma moja na likitengenezwa nchini gharama zinakuwa ni Sh 400,000 pekee baada ya Mradi kukamilika kiwanda hicho kitabaki kuwa ni mali ya Serikali ambayo ndiyo faida kubwa kuliko zote”alisema Mhandisi Kalist.

Faida nyingine kuutokana na ushauri wa wataalamu kwa  Serikali ni pamoja na kuvipa nafasi viwanda vya ndani kufanya kazi na Mkandarasi ambaye kwa sasa ananunua Saruji na Nondo kutoka nchini ambapo mara kadhaa wafanyabiashara  wamekuwa wakisafirisha zaidi ya behewa ishirini na kumuuzia Mkandarasi hivyo kuongeza pato la Taifa.

Imeelezwa kuwa kutokana na kusitishwa kwa ununuzi wa vifaa kutoka nje ya nchi kumekuwa na faida kubwa kwa Taifa kutokana na fedha nyingi kubaki ndani ya nchi hasa baada ya Mkandarasi kufanya ununuzi wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa Mradi huo

Kuhusu suala la ajira Mhandisi Christopher Kalist aliwaambia waandishi wa Habari kuwa Mradi wa SGR LOT 5 unaojengwa katika kipande cha Mwanza hadi Isaka chenye urefu wa Km 341 ikiwa ni km 249 njia kuu na km 92 njia za kupishania umeajiri watanzania wapatao 500 na wageni wakiwa ni 8% .

Hii ni fursa nzuri kwa taifa letu watanzania hususani kwa Serikali yetu kukubali kuendeleza Mradi mkubwa wa kimkakati utakaoleta manufaa makubwa tena kwa wananchi waishio kijijini ambapo fursa hizo ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya maji,barabara,Umeme,mazingira mazuri ya kibiashara nk.

 

Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi