Tunza Mazingira Group:Serikali na wadau tushikeni Mkono .
NA ANTHONY SOLLO MBOGWE.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Tunza Mazingira Group yenye Makao Makuu yake Wilayani Mbogwe Mkoani Geita Renatus Kilangi,amewaomba wadau wa Mazingira ikiwemo Serikali kukipa ushirikiano Kikundi hicho ili kukiwezesha kutekeleza majukumu yake kwa weledi.
Mwenyekiti huyo ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake waliofika kujionea namna kikundi hicho kinavyotekeleza majukumu yake Wilayani Mbogwe.
Kilangi amebainisha kuwa,katika kuhamasisha utunzaji wa Mazingira, Kikundi chake kimefanya kazi hiyo katika maeneo mbalimbali ya Migodi Wilayani Mbogwe.Kikundi cha Tunza Mazingira chini ya uongozi wa Mwenyekiti Renatus Kilangi kimekuwa kikifanya Shughuli zake kwa kushirikiana na Uongozi wa Mgodi wa Isanjabadugu Gold Mine ulioko Nyakafuru Wilaya ya Mbogwe MkoaniGeita takribani miaka saba (7) .
Kuhusu mafanikio Mwenyekiti huyo amesema Kikundi cha Tunza Mazingira Group Renatus Kilangi amesema wamefanikiwa kuajili Vijana wapatao 6 wasichana watatu (3)na vijana wa kiume (3).
Mpaka sasa kikundi hicho kinatarajia kupanua wigo wa utekelezaji wa majukumu yake kwa kwenda katika maeneo mbalimbali ya Migodi katika Wilaya ya Mbogwe.
Aidha Mwenyekiti huyo ameushukuru Uongozi wa Serikali kupitia Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Sakina Mohamed kwa namna wanavyoshirikiana na Asasi za Kiraia katika Wilaya ya Mbogwe kikiwemo Kikundi cha Tunza Mazingira Group.
“kipekee naushukuru Uongozi wa Serikali kupitia Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Sakina Mohamed kwa namna wanavyoshirikiana na Asasi za Kiraia katika Wilaya ya Mbogwe kikiwemo Kikundi chetu cha Tunza Mazingira Group,tunaamini kwa ushirikiano huu tutafika mbali katika kuijenga Mbogwe”alisema Kilangi.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Tunza Mazingira Renatus Kilangi akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Mji Mdogo wa Masumbwe Wilaya ya Mbogwe januari 7 2024 .Picha na Antony Sollo.
Licha ya Kikundi cha Tunza mazingira kufanya shughuli za Mazingira kikundi hicho kinajishughulisha na kutoa Elimu ya Mpiga kura katika Chaguzi mbalimbali zinazofanyika Kitaifa pichani ni wananchi wa Kata ya Lugunga Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita wakipata Elimu kupitia kwa wanakikundi cha Tunza Mazingira picha na mwaka 2020 Antony Sollo Katika hatua nyingine
Mwenyekiti huyo ameziomba Taasisi zinazohusika na masuala mazima ya Uhifadhi
zikiwemo TFS,TANAPA,TAWA pamoja na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Ngorongoro NCAA na
wadau wengine wa Misitu ndani nan je ya nchi kukitumia kikundi hicho kwa
kukipatia shughuli za kuhamasisha Utunzaji Mazingira katika maeneo mbalimbali
nchini.
“Niombe sana Taasisi
zinazohusika na masuala ya Uhifadhi kama TFS,TANAPA,TAWA Mamlaka ya Hifadhi za
Taifa Ngorongoro NCAA pamoja na wadau wengine wa Misitu ndani nan je ya nchi kukitumia
kikundi chetu ili kunusuru Mazingira yetu kwa kuwa Misitu ni UHAI”amesema
Kilangi.
Kuhusu ushiriki wa Kikundi cha
Tunza Mazingira katika shughuli zingine ukiachana na Mazingira Mwenyekiti
Kilangi alibainisha kwamba wanashirikiana na Serikali katika kutoa Elimu ya
Mpiga kura.


Chapisha Maoni