Top News

 Hawa ndiyo Vigogo waliofanikisha ujenzi wa Ofisi ya Chama cha Mapinduzi Mbogwe.

NA ANTHONY SOLLO MBOGWE.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Nicolaus Kasendamila akisisitiza jambo wakati wa Maadhimisho ya Miaka 47 ya CCM yaliyofanyika Kimkoa Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita Picha Na ANTHONY SOLLO 

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita Mathias Nyololo ameweka hadharani Orodha ya wanachama na wadau waliofanikisha ujenzi wa Ofisi ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mbogwe.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita akikabidhiwa Picha kama zawadi ya Kiongozi aliyetoa Hotuba nzuri zawadi iliyotolewa na Bwana Fagason Aron Masasi Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Fedha kupitia Kundi la Umoja wa Vijana Wilaya ya Mbogwe katika Sherehe ya Maadhimisho ya Miaka 47 ya CCM   yaliyofanyika Kimkoa Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita Picha Na ANTHONY SOLLO 

Aidha Mwenyekiti huyo wa CCM Wilaya ya Mbogwe alisema,Chama cha Mapinduzi kitajengwa na wana CCM wenye moyo huku akimtaja  Mbunge wa Jimbo la Mbogwe Nicodemus Henry Maganga,Evarist Gervas Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, George Patrick Msafi Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa,Fagason Aron Masasi Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Fedha kupitia Kundi la Umoja wa Vijana Wilaya ya Mbogwe kuwa kundi hili ndilo lililoonyesha upendo kwa Chama hicho.

Pichani ni Mbunge wa Jimbo la Mbogwe Nicodemus Henry Maganga akiwasalimia wananchi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi waliohudhuria katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 47 ya CCM yaliyofanyika Kimkoa katika Wilaya ya Mbogwe na Mgeni rasmi alikuwa ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Nicolaus Kasendamila Picha na ANTHONY SOLLO.

Akizungumza wakati wa Maadhimisho ya miaka 47 ya Chama hicho Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita Mathias Nyololo alisema kazi ya ujenzi wa Ofisi hiyo alikabidhiwa lakini hakuwa na Senti hata moja lakini walijitokeza wanachama wa CCM pamoja na wachimbaji wa Madini ambao nao wako katika historia ya waliofanikisha ujenzi wa Ofisi ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mbogwe.

Licha ya Orodha hiyo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbogwe Mathias Nyololo aliwashukuru wanachama pamoja na wadau wote waliofanikisha kwa namna moja au nyingine ujenzi wa Ofisi ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mbogwe.

“Mh Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi yapo mambo manne tuliyoelekezwa kuyafanya,jambo la kwanza ni ujenzi wa Ofisi za Chama cha Mapinduzi kwenye Wilaya kutoka Matawi mpaka Wilaya,napenda kutamka kwamba kazi hiyo tumeifanya kwa uaminifu mkubwa”alisema Nyololo.

Pichani ni Mwenyekiti wa CCM Nicolaus Kasendamila akimkabidhi Baiskeli mmoja wa Wenyeviti wa Shina waliotunukiwa zawadi ya Baiskeli kufuatia utendaji mzuri wa majukumu yao Picha na ANTHONY SOLLO. 

Akizungumza katika Maadhimisho hayo Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa alisema Chama pekee kilicho na uwezo wa kuwaongoza Watanzania ni Chama cha Mapinduzi tunaadhimisha miaka 47 ya CCM tukiwa na Ari kubwa tukiwa na Morari kubwa kwa sababu CCM ndiyo Chama pekee chenye uwezo wa kuongoza Serikali.

kwa jina naitwa Evarist Paschal Gervas Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ninayewakilisha Mkoa huu wa Geita,ndugu Mwenyekiti leo ni siku ya maadhimisho ya miaka 47 ya CCM tukiwa na Ari kubwa tukiwa na Morari kubwa kwa sababu CCM ndiyo Chama pekee chenye uwezo wa kuwaongoza watanzania Mil 61 wakiwemo wananchi wa Mbogwe”alisema Evarist Paschal Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi