Top News

NAIBU WAZIRI ENG KUNDO ,MBUNGE MAGANGA WAKAGUA UJENZI WA MRADI WA MAJI MBOGWE.


   

Mbunge wa Jimbo la Mbogwe Nicodemus Henry Maganga akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Ushirika wakati wa Mkutano wake ulioandaliwa kwa ajili ya ziara yake akiambatana na Naibu Waziri wa Maji julai 19 2024.



NA ANTHONY SOLLO MBOGWE

NAIBU WAZIRI wa Maji Eng Kundo Andrew amefanya Ziara katika Jimbo la Mbogwe Mkoani Geita ambapo pamoja na mambo mengine Waziri huyo ametembelea Jengo la Ofisi ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mbogwe lililoko Kijiji cha Kasosobe yaliko Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Mkoani humo na baadaye kukagua ujenzi wa Mradi wa maji ulioko katika Kata za Isebya na Ushirika Wilayani humo.

Akiambatana na Mbunge wa Jimbo la Mbogwe Nicodemus Maganga Naibu Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bariadi alishuhudia ujenzi wa Mradi wa maji katika Jimbo la Mbogwe ukienda kwa kasi na kumpongeza Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)Eng Rodrick Mbepera kwa usimamizi mzuri wa Mradi huo.

Hata hivyo Viongozi wa Chama cha Mapinduzi walimpongeza Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)Eng Rodrick Mbepera kwa usimamizi mzuri wa Mradi huo huku wakiomba aendelee kubaki katika Wilaya hiyo kwa kuwa kutokana na kuwaunganisha wafanyakazi wenzake na kufanya kazi kama Timu matokeo yake ndiyo chanzo cha mafanikio haya ya upatikanaji wa maji wa kuridhisha katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Mbogwe.

Akisoma taarifa Mbeya Naibu Waziri wa Maji,Meneja wa Ruwasa Eng Rodrick Mbepera alibainisha kwamba katika bajeti ya mwaka 2023/2024 Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)Mkoa wa Geita iliingia Mkataba wa ujenzi wa miundombinu ya Mradi wa Maji katika Vijiji vya Ikobe, Isebya, Ushirika na Mlale na Mkandarasi aitwae Otonde Construction & General Supplies Limited ya Mwanza.

Mhandisi Mbepera amesema Mkataba huu ulisainiwa mnamo tarehe 15/04/2024 na utatekelezwa kwa kipindi cha muda wa mwaka mmoja (Siku 365),na utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu hii ulianza rasmi mnamo tarehe 29/04/2024 na unategemea kukamilika mnamo tarehe 14/04/2025.

Mradi huu wa maji unategemea kuhudumia Vijiji sita (06) ambavyo ni Ushirika, Kadoke, Ushetu, Mlale, Ikobe na Isebya vilivyopo katika Kata ya Ushirika, Isebya na Ikobe ambapo chanzo cha maji cha Mradi huu ni visima Virefu vitatu (03) ambavyo vipo katika Kijiji chMlale na kina urefu wa mita 100 na uwezo wa kisima kutoa Maji ni lita 11,500 kwa saa, Kisima cha Maji Kijiji cha Isebya kina urefu wa mita 90 na uwezo wa kisima kutoa Maji ni lita 5,200 kwa saa, na Kisima cha Maji Kijiji cha Ikobe kina urefu wa mita 63 na uwezo wa kisima kutoa Maji ni lita 3,600 kwa saa. 

Mhandisi Mbepera ameeleza kuwa Serikali imetenga jumla ya Shilingi 2,050,923,546.11,pamoja na VAT kupitia fedha za Mpango wa Malipo kulingana na Matokeo (PforR) kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi huu ni ambapo hadi sasa Mkandarasi amekwisha lipwa jumla ya fedha kiasi cha Shilingi 1,385,589,283.62 kwa kazi alizofanya. 

Mbepera ameeleza pia kuwa kazi zilizokwishafanyika katika Ujenzi wa Mradi huu ujenzi wa nyumba kwa ajili ya Pampu moja (01), ujenzi wa vituo vya kuchotea maji kumi na saba (17), uingizaji wa miundombinu ya umeme kwenye nyumba ya Pampu pamoja na ufungaji wa pampu, uchimbaji wa mitaro na ulazaji wa bomba urefu wa Mita 20,719 na ujenzi wa daraja nane (08) za kupitisha bomba.

Kuhusu kazi zinazoendelea Mhandisi huyo amebaimisha kuwa ni pamoja na ujenzi wa tenki moja (01) la kuhifadhia maji lenye lita za ujazo 150,000 juu ya Mnara wa mita 9, Ujenzi wa uzio kwenye nyumba za Pampu, tenki na vituo vya kuchotea Maji,uchimbaji wa mitaro na ulazaji wa bomba urefu wa Mita 1,237,na kufanya ukamilishaji kwenye nyumba ya Pampu, tenki na nguzo za fensi kwa kupaka rangi.

Kwa upande wa Kata ya Isebya Mhandisi Mbepera alisema kuwa,kazi zilizokwishafanyika katika Ujenzi wa Mradi huu ni pamoja na ujenzi wa nyumba ya Pampu moja (01), Ujenzi wa tenki moja (01) la kuhifadhia maji lenye lita za ujazo 75,000 juu ya Mnara wa mita 9, ujenzi wa vituo vya kuchotea maji saba(7),uingizaji wa miundombinu ya umeme kwenye nyumba ya Pampu pamoja na ufungaji wa pampu, uchimbaji wa mitaro na ulazaji wa bomba urefu wa Mita 4,000 na ujenzi wa daraja sita (06) za kupitisha bomba.

Aidha katika kazi zinazoendelea ni pamoja na ujenzi wa uzio kwenye nyumba ya Pampu, tenki na vituo vya kuchotea Maji, uchimbaji wa mitaro na ulazaji wa bomba urefu wa Mita 819, kufanya ukamilishaji kwenye nyumba ya Pampu, tenki na nguzo za fensi kwa kupaka rangi.

Katika Kata ya Ikobe kazi zilizokwishafanyika katika Ujenzi wa Mradi huu ni pamoja na ujenzi wa nyumba ya Pampu moja (01), Ujenzi wa tenki moja (01) la kuhifadhia maji lenye lita za ujazo 50,000 juu ya Mnara wa mita 12, ujenzi wa vituo vya kuchotea maji sita (06), uingizaji wa miundombinu ya umeme kwenye nyumba ya Pampu pamoja na ufungaji wa pampu, uchimbaji wa mitaro na ulazaji wa bomba urefu wa Mita 5,000 na ujenzi wa daraja tano (05) za kupitisha bomba.

Kuhusu kazi zinazoendelea ni ujenzi wa uzio kwenye nyumba za Pampu,tenki na vituo vya kuchotea Maji,uchimbaji wa mitaro na ulazaji wa bomba urefu wa Mita 900, Kufanya ukamilishaji kwenye nyumba ya Pampu, tenki na nguzo za fensi kwa kupaka rangi.

Kutokana na kasi ya ujenzi huo hadi sasa ujenzi wa miundombinu ya Maji Katika Vijiji vya Ikobe, Isebya, Ushirika na Mlale umefikia asilimia 75%.

Kuhusu faida za Mradi Mhandisi Mbepera amesema Mradi huu utakapo kamilika utaendeshwa na Jumuiya ya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (CBWSO’s) ya Imalabupina - Nanda iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Na.5 ya mwaka 2019, ambapo itahusika na usimamizi, uendeshaji wa shughuli zote za Mradi na ukusanyaji wa fedha za mapato ya maji na kuziweka benki kwa ajili ya uendelevu wa Mradi huu.

Akizungumzia faida za Mradi Mhandisi Mbepera alisema baada ya kukamilika kwa Mradi huo wananchi takribani 21,009 waishio katika Vijiji vya Ushirika (3,624), Ushetu (2,837), Mlale (2,375), Kadoke (2,376), Ikobe (5,484) na Isebya (4,313) watapata huduma ya maji safi na salama na itawasaidia kupunguza kutumia muda mwingi kutafuta huduma ya maji hivyo muda huo utatumika katika shughuli za kiuchumi.

Faida nyingine ni kupunguza ongezeko la magonjwa ya milipuko kama vile Kuhara,Kipindupindu na homa ya matumbo kwa wananchi kutokana na uwepo wa huduma ya maji safi na salama huku faida nyingine ikiwa ni kupunguza mimba na utoro mashuleni kwa wanafunzi wa kike uliokuwa ukisababishwa na kufuata huduma ya maji mbali. 

MWISHO.

 

Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi