MADIWANI WASHTUKIA UPIGAJI WA MAPATO YA SERIKALI.
NA ANTHONY SOLLO MBOGWE.
KUFUATIA kudorora kwa ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri,Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita limeunda Kamati Maalumu ya ufuatiliaji wa Mapato ya Migodi iliyoko katika Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Kamati hiyo
inaongozwa na Mwenyekiti Marco John Nzella huku wajumbe wa Kamati hiyo
wakiwa ni pamoja na Lucy Samwel,Paul Edward Ngussa,pamoja na Mbunge wa
Jimbo la Mbogwe Nicodemus Maganga.
Kamati
hiyo pia imeambatana na Wataalamu kutoka Serikalini ambapo miongoni mwa
watumishi hao ni pamoja na Eng Yohana Marwa anayemwakilisha Ofisa
Madini Mkazi Mkoa wa Kimadini wa Mbogwe,Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya
ya Mbogwe pamoja na Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Mbogwe Nicodemus Henry Maganga akizungumza na wananchi katika Mgodi wa Isanjabadugu ulioko Nyakafuru.Wananchi wakimpokea kwa shangwe Mbunge wao baada ya kuwasili katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Nyakafuru Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita.
Mbunge wa Jimbo la Mbogwe akiteta Jambo na Mkurugenzi wa Mgodi wa Kanegele Namba moja Bwana Elias Kisome baada ya kuwasili akiambatana na Kamati Maalumu iliyoundwa na Madiwani kwa lengo la kufuatilia Mapato ya Halmashauri hiyo.
Wakiwa
katika Mgodi wa Kanegele Namba Moja Maarufu kwa mchungaji, Kamati hiyo
imepokelewa na kufanya majadiliano kwa saa kadhaa huku ikiomba taarifa
ya Mapato ya March 2024 ambapo Mkurugenzi wa Mgodi huo Elias Kisome
alijitetea mbele ya Kamati hiyo,kuwa kutokana na ajali iliyotokea katika
Mgodi huo shughuli za uzalishaji zilisimama.
Hata
hivyo Mkurugenzi wa Mgodi wa Kanegele Namba Moja Elias Kisome ameiambia
Kamati hiyo kuwa baada ya kuanza kwa shughuli za uzalishaji Mgodi huo
umelipa jumla ya Tshs Mil 8.kwa ajili ya maombi ya kupeleka mawe kwenye
Mtambo wa kisasa unaotumika kuchakata mawe yanayosadikiwa kuwa na
Dhahabu (CIP)
Baada ya
majadiliano na Kamati mjumbe wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Mbogwe Nicodemus Maganga alifanya mkutano na wachimbaji
wanaofanya shughuli zao katika Mgodi huo huku akihamasisha wananchi
kwenda kujiandikisha katika Vituo kwa ajili ya uboreshaji wa taarifa
katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura
Licha
ya kuhamasisha wananchi kwenda kujiandikisha katika Daftari la Kudumu
la Wapiga kura Mbunge Maganga alikaribisha wananchi kutoa maoni pamoja
kero ambapo Solomon Mathayo alimuomba Mbunge wa Jimbo la Mbogwe
Nicodemus Maganga kutumia nafasi yake kama mwakilishi wa wananchi
kuishawishi Serikali kufanya mabadiliko ya Sheria ya Madini.
"Nikuombe
sana mheshimiwa Mbunge wetu uende kuitumia nafasi yako kama mwakilishi
wa wananchi kuishawishi Serikali kufanya mabadiliko ya Sheria ya Madini
ili iweze kwenda na wakati maana sisi kama wachimbaji tunapata shida
kubwa hasa tunapogundua Madini katika maeneo yetu.
Katika
hatua nyingine akiendelea na ziara yake Mbunge wa Jimbo la Mbogwe
Nicodemus Maganga ameendelea na ufuatiliaji wa Mapato katika Mgodi wa
Migodi katika maeneo ya Mwagimagi na kuhitimisha ziara yake katika Mgodi
wa Nyakafuru na kisha kuzungumza na wananchi ambapo pia kilio Chao ni
utitiri wa Tozo za Halmashauri
Chapisha Maoni