NA ANTHONY SOLLO BUNGENI DODOMA
KATIKA Bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23 na 2023/24 Serikali kupitia Mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mbogwe ilipeleka shilingi mil 100 katika Kituo cha Afya cha Nhomolwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo la wagonjwa wa nje na nyumba ya mtumishi ya 2 in1,ambapo ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje umekamilika na Kituo kimeanza kutoa huduma mwezi Oktoba, 2023.
Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Geita Mheshimiwa Rose Busiga aliyetaka kujua ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje na nyumba ya Mtumishi ya 2 in1,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,(TAMISEMI),alisema katika mwaka wa fedha 2024/25 Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mbogwe imetenga Shilingi milioni 50 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa jengo la Maabara.
"Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,(TAMISEMI)naomba kujibu swali la MHESHIMIWA ROSE VICENT BUSIGA, MBUNGE WA VITI MAALUM Mkoa wa Geita kama ifuatavyo,Mheshimiwa Spika,Kituo cha Afya Nhomolwa kipo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe,Kituo hiki kilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi kwa kujenga jengo la kutolea huduma za nje (OPD) na majengo mawili ya wodi ya kulaza wagonjwa.
Mheshimiwa Spika,Serikali itaendelea kutenga fedha kwa awamu kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa majengo ya kituo cha Afya Nhomolwa na Serikali imesema katika bajeti ya 2024/25 itapeleka fedha za kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Nhomolwa”alisema Naibu Waziri huyo.

Chapisha Maoni