Wananchi wasema Waziri Biteko ameonyesha Umahiri Mkubwa Kiutendaji.
Kauli mbiu aliyoianzisha Maarufu (KNK) KUSEMA NA KUTENDA imejidhihirisha wazi.
NA ANTHONY SOLLO. GEITA
WAKAZI wa Mkoa wa Geita wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Uteuzi alioufanya kwa Kumteua Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dkt Doto Biteko kuwa Waziri wa Nishati na baadaye kumpa nafasi ya Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakizungumza katika mahojiano na Vyombo vya Habari wananchi hao wamempongeza Rais Dkt Samia kwa uamuzi wake kwamba ulifanyika kwa umakini mkubwa kwani Dkt Biteko anaweza kukijenga na kukiimarisha Chama hicho,kutokana na uwezo mkubwa pamoja na ushawishi alio nao kwa Jamii.

Kauli hiyo imetolewa na Wananchi wa maeneo mbalimbali ya Jimbo la Bukombe wakati wakitoa maoni yao mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu Mwenendo wa Chama cha Mapinduzi kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.
"Kipekee tunapenda kumpongeza Rais wetu Dkt Samia kwa uamuzi wake wa Kumteua Mbunge wetu wa Jimbo la Bukombe Mhe Dkt Doto Biteko kuwa Waziri wa Nishati na baadaye kumpa nafasi ya Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Rais alifanya uamuzi huu kwa umakini mkubwa,Dkt Biteko anaweza kukijenga na kukiimarisha Chama,kutokana na uwezo pamoja na ushawishi mkubwa alio nao kwa Jamii"anasema Samson Jackob mkazi wa Runzewe.
UWEZO WA DKT BITEKO TISHIO KWA WAPINZANI.
Kutokana na Mapokezi makubwa anayopewa Naibu Waziri Mkuu huyo kutoka kwa wananchi,wapenzi na wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi,ni wazi kwamba Kauli yake ya Kubeba vyote katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa itatimia ifikapo Nov 27 ambapo mpaka sasa kwa mujibu wa wananchi wenyewe wameridhishwa na Uwajibikaji wa Dkt Biteko na Chama cha Mapinduzi kwa ujumla.
GEITA YAITIKA ,DKT BITEKO ASOMBA KIJIJI.
Mara baada ya kuwasili Mkoani Geita Novemba 24, 2024 na kuhutubia katika Kampeni zinazoendelea za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Wilaya ya Geita zilizofanyika katika Viwanja vya Nyankumbu mkoani humo Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa CCM chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia imejipanga kuifanya Geita kuwa na maendeleo zaidi.
"wananchi wa Jimbo la Geita niwaombe sana katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaofanyika Novemba 27, 2024 ichagueni CCM na kuipa ushindi wa heshima.
Ninyi ni mashahidi mmeona jitihada za kuwaletea maendeleo zilizofanywa na CCM yote haya ni pamoja na juhudi za Rais Samia za kuhakikisha Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) unawanufaisha zaidi wananchi kwa Geita"anasema Dkt Biteko.

Aidha Waziri Biteko amezungumzia Miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa katika Mji wa Geita, kila kona huku akiwataka wananchi wawachague Viongozi watakaoshirikiana na viongozi wengine ili kutuletea maendeleo,na kusisitiza kuwa CCM inataka ushindi wa heshima.
“ Kwetu sisi hivi ni Vyama rafiki na Mhe. Rais anaeleza kuhusu falsafa ya 4R, tunataka tuiambie Afrika na dunia kuwa Tanzania ni nchi ya demokrasia na tunafuata misingi ya waasisi wetu na sisi Geita hatuta wabagua vyama vingine lakini jambo moja hatuna huruma nalo ni kura na hatuwapi kura hata moja,”
Biteko amesema “ CCM inabeba vyote, tunabeba vijiji, vitongiji na mitaa yote hatuwaachi hata kimoja na tunafanya hivyo kwa sababu wananchi wameridhishwa na kazi kubwa ya miradi ambayo CCM imetekeleza hapa na inaendelea kutekeleza.
Aidha, Dkt. Biteko amesema kuwa Serikali imefanya jitihada kubwa za kuhakikisha Tanzania inaendelea kuimarika kiuchumi kwa kuanzisha miradi ya umeme ambayo imeongeza utoshelevu wa umeme nchini pamoja na uwepo wa treni ya umeme ambayo imeanza safari zake kutoka Dar es salaam hadi Dodoma na inatarajiwa kufika Burundi hapo baadae.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini, Mhe. Constantine Kanyasu amesema kuwa Wilaya ya Geita imejipanga kushinda katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuwa wananchi wameona miradi ya maendeleo inayotekelezwa wilayani humo.
Hata hivyo, Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Mhe Constantine Kanyasu ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Afya, Elimu na Barabara ambayo inaendelea vizuri.
Naye Mbunge wa Jimbo la Busanda, Mhe. Tumaini Magesa amewahimiza wananchi wa Geita kuwapigia kura wagombea wa CCM kwa kuwa Serikali ya Rais Samia ina nia ya dhati ya kuwaletea maendeleo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Geita, Barnabas Mapande amesema kuwa Wilaya yake ina vijiji 158, Mitaa 65 ambapo vyama vingine vimeweka wagombea 50 na nane kati yao hawataendelea kugombea, katika vitongoji 640 vyama vingine vimeweka wagombea 115 ambapo 92 kati yao wameandika barua ya kutoaendelea na vyama hivyo na kwamba wagombea wa Vyama hivyo wamefikia uamuzi huo baada ya kuona jitihada za CCM za kuleta maendeleo katika wilaya hiyo.

Chapisha Maoni