
NA MWANDISHI WETU CHALINZE
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete ameongoza Matembezi yanayojulikana kama Sunset Walk kuunga mkono Taasisi hiyo ambayo inasimamia Haki za wenye Ualbino (TAS) na Rotary Club ili kuchangia Fedha kusaidia kupatikana kwa mahitaji muhimu kama Mafuta ya Ngozi na kofia kinga.
Katika hotuba yake,Waziri Kikwete amewakumbusha juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali ikiwemo mpango kazi wa kupambania Haki za wenye Ulemavu wakiwemo wenye Ualbino utakao zinduliwa hivi karibuni.




Chapisha Maoni