Top News

SIMBA KUUMANA NA WAMISRI HATUA YA ROBO FAINALI

 Hatimaye droo ya kupangwa michezo ya hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Ligi ya Shitrikisho barani Afrika imepangwa rasmi huku timu pekee kutoka nchini Tanzania na Afrika Mashariki na Kati, Simba SC ikipangwa kucheza dhidi ya klabu ya Al Masry ya nchini Misri ambayo kwasasa inashika nafasi ya nne kwenye ligi kuu nchini humo. Mchezo wa kwanza Simba SC watatakiwa kuifata klabu hiyo nchini Misri kisha mchezo wa pili utachezwa kwenye ardhi ya Tanzania.

Endapo Simba itafanikiwa kushinda na kuvuka kwenye hatua hiyo basi itakcheza hatua ya nusu fainali kati ya Zamalek ya nchini Misri au Stellenbosch ya nchini Afrika Kusini.



Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi