Top News

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ELIMU UTAMADUNI NA MICHEZO YAITAKA SERIKALI KUHARAKISHA UKARABATI UWANJA WA MKAPA.

NA ANTHONY SOLLO BUNGENI DODOMA.

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imeiomba Serikali kuharakisha Mradi wa  Ukarabati wa uwanja wa Benjamin Mkapa na kuhakikisha unakamilika ifikapo Aprili 2025, ili uweze kukidhi Viwango vya Killmataifa kwa ajili ya mashindano ya CHAN na AFCON 2027 yanayotarajiwa kufanyika Nchini Tanzania. 
Published from Blogger Prime Android App

Pichani ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo Mh  Husna Sekiboko,akiwasilisha Taarifa ya Shughuli za Kamati hiyo kwa mwaka wa Fedha 2024 hadi 2025, katika Kikao cha Bunge kilichofanyika leo Februari 11, 2025  jijini Dodoma.

Azimio hili limetolewa na wakati Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mh  Husna Sekiboko, alipokuwa akiwasilisha Taarifa ya Shughuli za Kamati hiyo kwa mwaka wa Fedha 2024 hadi 2025, katika Kikao cha Bunge kilichofanyika leo Februari 11, 2025  jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh Husna, Sekiboko aliipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuziongezea Bajeti Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Habari, Utamaduni na Michezo, jambo lililosaidia kufanikisha utekelezaji wa Miradi mingi kwa ufanisi. 

Hata hivyo Mh Sekiboko , aliiomba Serikali kuhakikisha inatekeleza Miradi inayoendelea kwa wakati ili kuleta maendeleo ya haraka kwa Taifa na Jamii kwa ujumla.
Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App

Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi