Mbunge wa Jimbo la Msalala ahamasisha UWT kuibua Miradi.
Na
AntonySollo - MSALALA.
Mbunge Iddi alitumia nafasi hiyo kuwapongeza akina mama hao kwa kubuni na kuanzisha Saccos ijulikanayo kwa jina la (WANAWAKE SHOKA) ambayo itawasaidia wanawake kujikimu mahitaji yao ya msingi pindi watakapoanza kazi za uchimbaji wa kokoto.
"Akina mama mmefanya kazi kubwa ya
ubunifu wa kuanzisha Saccos hii, niwaombe mshikamane na pendani,achaneni na
maneno kwa kuwa yanaweza kuwasababishia matatizo ya kuwafanya kuyumba kiuchumi"alisema
Iddi Kassim Iddi Mbunge Jimbo la Msalala.
"mimi nimeteta na Mkurugenzi,lengo ni kutaka kikundi chenu kiweze kukopeshwa fedha kiasi cha Sh milioni 300 hadi 400 ambazo zitawasaidia kuwa na mashine za kisasa,tunatambua Mradi huu ni mkubwa tunataka huko mbele muajili watu wengine"alisema Iddi Kassim Iddi Mbunge Jimbo la Msalala.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala Florah Sagasaga alitumia nafasi hiyo kumshukuru Mbunge Jimbo la Msalala Iddi Kassim kwa namna alivyoweza kuwasaidia akina mama hao kufikia lengo la kuanzisha Saccos hiyo ambayo imesajiliwa kwa mujibu wa Sheria.
Naye Katibu wa UWT Wilaya ya Kahama Happynes Charles aliwataka wanawake hao wa Jumuiya ya wanawake kujitolea kwa nguvu zao zote ili waweze kuendeleza jitihaza za Kikundi hicho.
MWISHO.
Chapisha Maoni