Mfumo wa Stakabadhi
ghalani kuondoa changamoto ya wakulima kukopwa Mazao yao.
Na Antony Sollo
DODOMA.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika ukumbi wa Idara ya
Habari Maelezo Jijini Dodoma Bangu alisema kuwa dhumuni la Kuanzishwa kwa Mfumo
wa Stakabadhi za Ghala ni kukuza juhudi za Serikali,kurasimisha mifumo ya
masoko iliyopo kwa lengo la kupunguza vipingamizi mbalimbali vinavyokwaza
uzalishaji wenye tija na utafutaji masoko kwa bidhaa mbalimbali hususan mazao
ya kilimo
Mkurugenzi huyo alieleza kuwa,Mfumo huu una manufaa makubwa ikiwemo kuwapa nguvu waweka mali hususani wakulima kupigania bei nzuri katika soko kwa kuhamasisha kutumia mfumo wa pamoja kukusanya na kuuza, kutoa uhakika wa ubora na bidhaa na Mfumo wa uthibitisho na kupunguza mashaka na gharama za ushughulikiaji.
Hurahisisha pia kuondoa mashaka kwa
wafanyabiashara wa bidhaa na wakulima wakati wa kufanya biashara kuweka utaratibu
wa kupata taarifa takwimu za soko na mauzo,taarifa za kuaminika kwa wadau
mbalimbali kuongeza ushiriki wa wafanyabiashara wa bidhaa wenyeji katika
biashara ya kimataifa,kuhimiza usindikaji wa mazao ya msingi kwa lengo la
kuongeza thamani na kukuza uendelezaji wa viwanda.
kuongeza upatikanaji wa sehemu za
kuhifadhia mazao zilizo bora, kupunguza hasara za baada ya kuvuna na kuimarisha
uhakika wa upatikanaji wa chakula na kuongeza wigo wa wananchi kuweza kukopa
katika asasi za fedha kwa kutumia mazao yao kama dhamana.
Akizungumzia Utekelezaji wa mfumo huo
nchini Tanzania Bangu alisema kuwa Kufuatia vikwazo mbalimbali katika mauzo ya
bidhaa za wazalishaji wadogo hususan mazao ya kilimo nchini mwaka 1999 Serikali
iliendesha mradi utafiti wa mbinu bora ya kuwawezesha wakulima kupata bei nzuri
katika mazao kupitia ukusanyaji wa pamoja na kuuza kwa njia ya Stakabadhi ya
Ghala.
Baada ya kufanikiwa kwa majaribio
hayo, mwaka 2005 Sheria ya Stakabadhi za Ghala ilipitishwa na Bunge na kuanza
kutumika katika msimu wa mwaka 2007/8 katika zao la korosho.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa tangu
kuanza kutumika kwa Sheria ya Stakabadhi za Ghala, mfumo umetekelezwa katika
mazao 11 yaliyoleta makusanyo zaidi ya kilogramu bilioni 2.3 hadi kufikia Robo
ya Kwanza ya Mwaka 2021/22.
Kuhusu Mafanikio Bangu alisema
kuwa,katika Mazao mbalimbali mafanikio yaliyopatikana baada ya kuanzishwa kwa
Mfumo wa Stakabadhi za Ghala ni pamoja na (i) ongezeko bei la bei za mazao,
mapato ya mkulima na mapato ya Serikali kwa wastani wa asilimia 200% kutokana
na urasimishaji.
Mafanikio mengine ni pamoja na ongezeko la uzalishaji wa mazao kwa wastani wa asilimia 12% kwa mwaka,kichocheo cha ubora wa mazao yanayofikishwa sokoni,upatikanaji wa takwimu sahihi za mazao yanayopita kwenye Mfumo wa Stakabadhi za Ghala,ongezeko la mapato ya uhakika kwa Serikali Kuu na Serikali Mitaa,kukuza huduma za fedha vijijini ili kufanikisha uanzishaji wa Soko la Bidhaa Tanzania.
Kuhusu zao la Korosho Mkurugenzi huyo alisema kuwa baada ya kuanzishwa kwa Mfumo, mwenendo wa bei na ushalishaji ulibadilika ghafla na kuanza kuwa na mwenendo chanya positive trend ambapo mara baada ya kuanzishwa kwa Mfumo palikuwa na ongezeko la asilimia 164% la bei kutoka Ths 350.00 msimu wa 2006/07 hadi kufikia Tsh 925.00 msimu wa 2007/08.
Hata hivyo Bangu alisema tangu kuanza kwa Mfumo katika miaka minane ulipoanzishwa Mfumo huu kwa maana ya 2007/08 hadi 2014/15 wastani wa ongezeko la bei kwa mwaka ulikuwa 25% kulinganisha na ongezeko la bei miaka minane kabla ya kuanzishwa kwa Mfumo ambapo ilikuwa ni asilimia 12% kwa mwaka kaunzia mwaka 1998/99 hadi 2006/07.
Chapisha Maoni