Miradi ya kimkakati yazalisha ajira 1,770 kwa Wazawa.
Na Antony Sollo DODOMA
KUFUATIA Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuendeleza ujenzi wa Miradi ya kimkakati nchini iliyokuwa ikijengwa na Mtangulizi wake aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt John Pombe Magufuli zaidi ya Watanzania 83,000 wamepata ajira.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Jijini Dodoma Februari 14, 2023 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa amesema kuwa,kupitia Miradi hiyo watanzania wapatao83,000 wamepata ajira.
Akitoa taarifa ya utakelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’I Issa alisema Baraza lina majukumu ya kuwezesha kubuni,kupanga, kusimamia,kufuatilia,kutathmini na kuratibu shughuli zote za uwezeshaji wa kiuchumi nchini.
Katibu Mtendaji wa baraza la
uwezeshaji Beng’i Issa aliseama kuwa,Baraza hilo pia lina jukumu la kusimamia
na kuratibu Mifuko na Programu za uwezeshaji na kwamba hadi sasa kuna Mifuko
zaidi ya 72.
Katibu huyo pia alisema baraza la uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) linasimamia programu za uwezeshaji (Viwanda Scheme)ambapo wafanyabiashara wenye viwanda vidogo na vya kati hukopeshwa.
"Hadi sasa baraza hilo limewezesha
wafanyabiashara wenye viwanda vya kati na vidogo katika miradi 62 kupatiwa fedha
zaidi ya Shilingi bil 3.5 kwenye
Mikoa 12 nchini,"alisema Beng’i.
Chapisha Maoni