NCC yaanika Mipango ya utekelezaji kwa mwaka wafedha 2022/2023.
Na Antony Sollo - DODOMA.
MTENDAJI Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (National Construction Council)Matiko Mturi amesema kuwa,kwa mwaka wa fedha 2022/2023 baraza hilo lilikusudia kutekeleza kazi muhimu mbalimbali nchini ili kutimiza malengo yake.
Akizungumza na Waandishi waHabari katika Ukumbi wa Habari Maelezo Jijini Dodoma Mturi alisema Baraza la Taifa la Ujenzi lilikusudia kutekeleza mambo mbalimbali ikiwemo kukamilisha muongozo wa gharama za Ujenzi wa barabara nchini kwa kuandaa gharama za Msingi za Mkandarasi katika kutekeleza kazi mbalimbali za Ujenzi wa barabara kwa kila Mkoa Tanzania Bara.
Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na kuandaa mapendekezo ya kuboresha Sheria na Miongozo inayosimamia Ujenzi wa majengo nchini,kuandaa viwango msawazo vya majengo ya Serikali,kutoa mafunzo ya kujenga uwezo wa wadau wa Sekta ya ujenzi nchini.
Kwa mujibu wa Mturi, Baraza la Taifa la Ujenzi lilikusudia pia kutoa Fahirisi za bei (price indices) za vifaa,Mitambo na ujira katika shughuli za ujenzi kwa kila mwezi ili kuonesha mabadiliko ya bei ya vifaa vya ujenzi,kusimamia utatuzi wa migogoro inayotokea katika Miradi ya Ujenzipamoja na kutoa ushauri wa kiufundi kwa wadau mbalimbali wa Sekta ya ujenzi
Katika hatua nyingine Baraza la Taifa la Ujenzi lilikusudia kuanza maandalizi ya kuwa na wiki ya Ujenzi nchini pamoja na kukamilisha maandalizi ya Kanuni za utekelezaji wa Sheria ya Baraza (Cap162RE 2008)
Akizungumzia utekelezaji wa malengo hayo Mtendaji
wa Baraza la Taifa la Ujenzi Matiko Mturi alisema,katika kipindi cha mwaka wa
fedha 2022 kuanzia januari mosi hadi januari 2023 baraza hilo limefanikiwa
kutekeleza mipango yake.
Mturi alisema mipango iliyotekelezwa na baraza hilo ni pamoja na kuandaa rasimu ya mapendekezo ya gharama za msingi za ujenziwa barabara (base Unit rates)kwa kila Mkoa Tanzania bara na kuwakilisha katika kikao cha wadau wa ndani ya Serikali ili kupata maoni na ushauri wao.
Hata hivyo Mtendaji wa Baraza la Taifa la Ujenzi alisema kuwa mambo mengine yaliyotekelezwa na baraza hilo ni pamoja na kuratibu, kuandaa na kuwasilisha Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Andiko Dhana (Concept Note) lenye mapendekezo ya kuboreshwa kwa mfumo wa Sheria zinazosimamia ujenzi wa nyumba na majengo nchini.
Baraza hilo pia
limeratibu na kukamilisha matayarisho ya awali ya kuandaa Miongozo ya ujenzi wa
majengo nchini (Building Codes)matayarisho ya awali ya kuandaa Viwango na
Viwango Msawazo vya Majengo, Nyumba na Samani za Serikali kuendesha mafunzo ya
Kusimamia Mikataba ya Ujenzi na Utatuzi wa Migogoro katika miradi ya ujenzi kwa
wadau 155 kutoka Tanzania Bara na Tanzania Visiwani
Hata hivyo Dr Matiko Mturi aliwaambia
waandishi wa Habari kuwa NCC Imekusanya
takwimu, kuchakata na kutoa Fahirisi za bei za vifaa vya ujenzi (construction
materials and labour price indices) kwa kila mwezi na kutoa ushauri wa
kitaalamu kwa Taasisi mbalimbali hususani katika usimamizi wa mikataba ya
ujenzi na tathmini ya gharama na ubora wa ujenzi.
Dr Matiko Mturi alizitaja baadhi ya Taasisi
zilizopatiwa ushauri wa kitaalamu kuwa nipamoja na,Wizara ya Maji,Wizara ya
Afya,Mfuko wa Taifa wa Hifadhi
ya Jamii (NSSF),Mamlaka ya
Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA),Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa
Umma (PPRA),Mamlaka ya Majisafi
na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA),Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU).
Mtendaji huyo alisema kuwa taasisi zingine ni pamoja na Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO),Tume ya Utumishi wa Waalimu (TSC),Kampuni ya Petra Constrution
Co. Ltd na,Kampuni ya TEKNICON Ltd na kwamba baraza
hilo linaendelea kuratibu
utatuzi wa migogoro ya miradi ya ujenzi kwa njia ya adjudication na arbitration
ambapo jumla ya mashauri(6)yametolewa uamuzi na
31 yanaendelea katika hatua mbalimbali za utatuzi na kwamba hadi sasa baraza
hilo limekamilisha Rasimu ya Kanuni za utekelezaji wa Sheria ya NCC (Cap. 162
R.E. 2008).
Kuhusu Mipango ya Utekelezaji kuanzia
Februari mosi 2023 hadi juni 30 2023 Dr Mturi alisema baraza hilo limekamilisha Kuandaa Mapendekezo ya gharama za
Msingi za Ujenzi wa Barabara (base unit rates) kwa kila mkoa wa Tanzania Bara na kupata maoni na ushauri ya wadau wa
nje ya serikali hususani wakandarasi na washauri elekezi (consultants) ;
baraza pia limeandaa na kuwasilisha Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi(Sekta ya Ujenzi)
Mapendekezo ya Miongozo ya ujenzi wa majengo nchini(Building Codes)na kukamilisha kuandaa Viwango na Viwango Msawazo vya Majengo,Nyumba na
Samani za Serikali(Standards and Specifications for Government Buildings and Furniture).
Katika hatua nyingine baraza la Taifa la ujenzi
limeweza kutoa mafunzo ya Kusimamia Mikataba ya Ujenzi na Utatuzi wa Migogoro
katika miradi ya ujenzi kwa wadau wa sekta ya ujenzi hususani taasisi za umma
zinazotekeleza miradi ya miundombinu;
Baraza limeendelea kukusanya takwimu, kuchakata na
kutoa Fahirisi za bei za vifaa vya ujenzi (construction materials and labour price indices) kila mwezi kutoa
ushauri wa kitaalamu kwa wadau wa sekta ya ujenzi kuanza maandalizi ya awali ya
Wiki ya Ujenzi nchini inayotegemewa kufanyika mwezi Septemba mwishoni au Oktoba
mwanzoni.
Akizungumzia mwelekeo wa taasisi katika kutekeleza majukumu yake Dr Mturi
alisema kuwa baraza hilo pia lina wajibu wa
kufutilia
utekelezaji wa Sera ya Ujenzi nchini,kuandaa na kutekeleza Mpango Mkakati wa
Maendeleo wa Sekta ya Ujenzi.
Vilevile baraza litaendelea kutoa Miongozo mbalimbali ya Kitalaam (Technical Guidelines) ya maeneo
mbalimbali ya ujenzi ambapo Dr Mturi pia
aliwaambia waandishi wa Habari kuwa baraza pia limekusudia kuanzisha wiki ya huduma ya Sekta
ya ujenzi kwa wakati mmoja.
Baraza pia litaanzisha kongamano la wadau wa ujenzi kwa lengo la kuimarisha
uhusiano, ushirikiano ili kuongeza ubunifu na Teknolojia miongoni mwa wadau
katika sekta hii.
Lakini pia baraza litaendelea
kutoa mafunzo kwa wadau wa Ujenzi kuhusu Maadili na Utekelezaji wa miradi ya
ujenzi, sanifu-jenga na Usimamizi wa mikataba ya Ujenzi kwa wadau mbalimbali
kutoa mafunzo yanayolenga kukuza na kujenga wataam
mahiri katika Sekta ya ujenzi na kuanzisha Kituo cha Taarifa za Sekta ya Ujenzi
ambacho kitakuwa muhimu sana kwa wadau kupata taarifa muhimu za sekta ya ujenzi
ikiwa ni pamoja na kuendeleza tafiti, teknolojia na ubunifu.
Baraza pia litaendelea kuimarisha utoaji wa miongozo ya gharama za ujenzi
nchini,kuanzisha mfumo wa Kuboresha utendaji kazi wa Mafundi Stadi (skilled labourers)
katika sekta ya ujenzi,kuendelea kutekeleza maelekezo ya Serikali ya kisheria,
kikanuni, sera, mipango, miongozo na maelekezo yaliyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya 2020.
Chapisha Maoni