Tatizo Uhaba wa Mafuta lawaibua wabunge.
NA ANTHONY
SOLLO - DODOMA. 05.Sept 2023
WAKATI Vikao vya Bunge
vikiendelea Jijini Dodoma Wabunge wameishauri Serikali kutafuta namna bora ya
kukabiliana na changamoto ya uhaba wa Mafuta inayoendelea katika maeneo
mbalimbali nchini.
Wakizungumza na waandishi wa
Habari katika viunga vya Bunge Jijini Dodoma Wabunge hao
wamekiri kuwepo kwa uhaba wa mafuta katika maeneo mbalimbali nchini n ahata
katika majimbo yao.
Mbunge
wa Jimbo la Ngorongoro Emmanuel Oleshangay alisema hali ya ukosefu wa
mafuta inaathiri uchumi wa wananchi pamoja na Taifa kwa ujumla wake na kuongeza
kuwa katika Jimbo hilo ni vituo viwili tu vya mafuta vinavyotoa huduma hiyo lakini kwa muda wa takribani wiki mbili sasa
hawapati mafuta ya Petrol na hata Dizeli.
Aidha Mbunge huyo wa Jimbo la
Ngorongoro Emmanuel Oleshangay alisema kuwa kazi ya wabunge ni kuisimamia na
kuishauri Serikali,hasa katika masuala ya maendeleo ya nchi pamoja na yale ambayo
yanawaumiza wananchi hata hivyo Mbunge huyo aliishauri Serikali kutafuta
muarobaini ili kuona namna namna nzuri ya kuagiza mafuta kupitia (BPA) Bulc Procurement
Argency na pia aliishauri Serikali iweke akiba ya mafuta yatakayokuwepo angalau
kwa kipindi cha miezi sita ili kukabiliana na tatizohilo.
“Ni kweli kuna uhaba mkubwa wa mafuta ya Petroli na hata Dizeli,na mara kadhaa kama Wabunge tulishalitolea taarifa jambo hili kwa kuishauri Serikali iweke akiba ya mafuta angalau kwa kipindi cha miezi sita hivyo tunaendelea kuishauri itafute namna bora ya kukabiliana na tatizo hili”alisema Oleshangay.
Kwa upande wake Mbunge wa
Jimbo la Geita Mjini Costantine John Kanyasu ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya
Nishati na Madini alipotakiwa kutolea ufafanuzi kuhusu uhaba wa mafuta maeneo
mbalimbali nchini likiwemo Jimbo la Geita Mjini Mbunge huyo pia alikiri kuwepo
kwa changamoto hiyo.
Tatizo hili la uhaba wa
mafuta linalotokea mwezi huu wa tisa kama wabunge tulilijua tangu mwezi wa saba
kutokana na trend ya uingizaji wa mafuta lakini pia na trend ya uhaba wa fedha
za kigeni (USD)
“sisi kama Wabunge jambo hili
linatusikitisha sana kwa sababu linaathiri mfumo mzima wa uchumi wa wananchi wet
una kusababisha kupanda kwa gharama za Maisha “alisema Kanyasu.
Kanyasu amesema,kutokana na
uhaba wa mafuta wananchi wanapokosa mafuta katika vituo vya mafuta
vilivyosajiliwa kihalali wanalazimika kwenda kununua mafuta hayo kwa walanguzi badala
ya Sh 3400/3500 wananunua kwa gharama kati ya Sh 4500
hadi 5000.
Kwa hiyo hili ni jambo kubwa
linaathiri uchumi katika Nyanja zote ikiwemo usafiri,gharama za bidhaa na Maisha
yanapanda,kanyasu alisema,jambo la msingi ni kwamba tatizo hili ni la kidunia (Global)
ambalo linaanza na kuyumba kwa Uchumi wa Dunia lakini pia ni pamoja na vita
vinavyoendelea.
Mbunge huyo ambaye pia ni
mjumbe wa Kamati ya Nishati na Madini alisema Kamati hiyo imeishauri Serikali kutafuta kila aina ya mbinu za
kukabiliana na tatizo hili ikiwemo kutafuta msaada kwa nchi marafiki ,Akiba
zilizopo katika nchi na kutumia bidha zilizopo nchini ili kuweza kulimaliza
tatizo hili.
“Mfano mpaka sasa
tunavyoongea mafuta yabo Bandarini lakini hayawezi kushushwa kwa sababu mwenye
meli anataka alipwe fedha zake kwanza na kinachopelekea kutoshushwa kwa mafuta
hayo ni kutokana na uhaba wa dola”alisema Kanyasu.
Kuhusu Halmashauri
zilizofikia hatua ya kutokopesheka kutokana na kudaiwa madeni na wauzaji wa mafuta,Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Costantine John Kanyasu alisema
kuwa,Halmashauri ya Mji wa Geita ina viongozi mahiri wakiwemo
Madiwani wa Halmashauri hiyo ambao wanatekeleza vizuri majukumu yao kwa
uaminifu mkubwa huku akimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Zahara Muhidin Michuzi kwa
usimamizi mzuri matumizi ya fedha za Serikali.
Mbunge wa Jimbo la Geita
Mjini Costantine John Kanyasu Picha na Maktaba.
Chapisha Maoni