Top News

Makala kuhusu miaka miwili ya Rais Dkt Samia Suluhu na utekelezaji Miradi ya Kimkakati.

            

Makala kuhusu miaka miwili ya Rais Dkt Samia Suluhu na utekelezaji Miradi ya Kimkakati.

 

SGR LOT 5 kazi inaendelea Mradi haujasimama.

 

NA ANTHONY SOLLO MWANZA.

 

WAKAZI wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza Miradi ya kimkakati iliyoanzishwa na mtangulizi wake Hayati Dkt John Pombe Magufuli.

 

Miradi hiyo ni ile iliyoanzishwa kipindi cha awamu ya Tano na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt John Pombe Magufuli miradi ambayo ni pamoja na ujenzi wa Daraja la JPM lililoko Ziwa Victoria huko Kigongo Busisi Jijini Mwanza,Bwawa la Mwalimu Nyerere lililoko Rufiji Mkoani Pwani.

 

Baada ya kifo cha Hayati Dkt John Pombe Magufuli na nafasi yake kuchukuliwa na Rais Dkt Samia yapo mengi yaliibuliwa na wachambuzi wa kisiasa ikiwemo utabiri wa kutoendelezwa kwa Miradi jambo ambalo Rais Samia aliweza kuonyesha nia thabiti ya kuendeleza kwa kasi Miradi ya kimkakati iliyoachwa na Mtangulizi wake huyo.

 

Kutokana na juhudi zinazofanywa na Rais Samia,katika kuhakikisha utabiri wa wachambuzi unashindwa kutimia,mpaka sasa Rais Samia ameendelea kuisimamia Miradi yote iliyoanzishwa na Hayati Dkt John Pombe Magufuli ambapo Mradi wa Kufua Umeme wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP)umekamilika kwa asilimia 78.68 huku hatua ya kufunga lango la njia ya mchepusho wa maji ikiwa imefikiwa kwa lengo la kuruhusu ujazaji maji katika bwawa tayari kwa umeme kuanza kuzalishwa.

 

Kwa mujibu wa taaifa ya Msemaji wa Serikali bwawa Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP)linatarajiwa kukamilika na kuanza uzalishaji Juni mwaka 2024 na litagharimu Sh Tril 6.5.

 

Hivi karibuni Rais Samia Suluhu Hassan alizindua hatua ya kuanza ya kujaza maji katika bwawa hilo lenye ukubwa wa Meta za ujazo 32.3, hafla iliyofanyika katika eneo la Mardi huo, Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani.

 

Mradi mwingine ni ujenzi wa Reli ya mwenda kasi SGR vipande sita kuanzia Dar Es salaam Morogoro na Morogoro hadi Tabora na Kipande cha Mwanza Isaka na Isaka Tabora hadi Kigoma.

 

Akizungumza na waandishi wa Habari waliotembelea Mradi ujenzi wa Reli ya Mwendokasi SGR LOT 5 kipande cha Mwanza Isaka mwezi mei 2023 Mhandisi Moga Kulwa alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha za kumlipa Mkandarasi kwa wakati na kusema kuwa Mradi huo unaendelea vizuri na utakamilika kwa wakati.

 

Mhandis Moga aliwataka Watanzania kuendelea kuiamini Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan hasa katika usimamizi wa Miradi ya kimkakati ukiwemo ujenzi wa Reli kipande cha Mwanza Isaka.

 

Licha ya mafanikio makubwa katika ujenzi wa Miradi mikubwa ya kimkakati wananchi wameipongeza Serikali kwa kutenda Haki hasa katika ulipaji wa  malipo ya Fidia kwa wananchi waliopitiwa na Mradi wa Reli ya Kisasa.

 

Wananchi hao walieleza mafanikio makubwa ya kiuchumi waliyoyafikia kutokana na kulipwa fidia ya kupisha ujenzi wa Mradi wa Reli ya Mwendokasi ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba za kisasa,pamoja na kufungua biashara.

 

"Tuna  kila sababu ya kuishukuru Serikali kwa kututendea Haki kwa kutulipa fedha kwa thamani ileile baada ya kupisha ujenzi wa Reli kipande cha Mwanza Isaka,hatukuweza kushuhudia migogoro jambo ambalo limeleta faraja kwetu"alisema Maziku mkazi wa Isaka. 

 

 

Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi