Top News

Viongozi wa Madhehebu ya Dini wampongeza Mbunge Maganga.

NA ANTHONY SOLLO - MBOGWE.

VIONGOZI wa Madhehebu ya Dini Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Mbogwe Nicodemus Henry Maganga kwa kuwaunganisha wananchi wa Jimbo hilo katika Sherehe za kuuaga mwaka 2023 na kuukaribisha mwaka Mpya 2024.

Hayo yamebainishwa wakati wa Sherehe hizo zilizoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Mbogwe ambaye aliwaalika wananchi wote wa Jimbo la Mbogwe wa makundi mbalimbali zikiwemo Taasisi za Umma ili kuungana na familia ya Mbunge huyo katika kuadhimisha na kuukaribisha mwaka mpya 2024.

 hizo zilifanyika katika Viwanja vya Maganga Stadium  zilizopo Kata ya Nyakafuru na hudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali ngazi ya Wilaya na Mkoa ambapo Mgeni rasmi katika Sherehe hizo alikuwa ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Dotto Mashaka Biteko ambaye alimpongeza Mbunge huyo kwa kutimiza ahadi yake aliyoitoa katika Sherehe zilizofanyika Nyumbani kwake katika Jimbo la Bukombe mwaka 2023.

“Wana Mbogwe niwaombe sana mtengenezeni Mbunge wenu huyu aendelee kuwa mwakilishi,sisi kama Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunamuelewa vizuri kuhusu misimamo yake kuhusu kulisimamia jambo ambalo analifahamu”alisema Dkt Biteko.

Aidha Naibu Waziri Mkuu huyo alisema Mbunge huyo ni mtu makini,na pale ambapo haelewi huwa hasiti kuuliza ili aeleweshwe na akielewa hujiamini Zaidi na kufanya mambo makubwa.

Katika hatua nyingine Mbunge wa Jimbo la Mbogwe aliwashukuru wananchi wa Jimbo la Mbogwe kwa kujitokeza kumuunga mkono katika Sherehe aliyoiandaa ili kushirikiana katika kuuaga mwaka 2023 na kuukaribisha mwaka mpya 2024.

“binafsi napenda kuwashukuru sana wananchi wa Jimbo langu la Mbogwe pamoja na wageni mbalimbali nmliohudhuria Sherehe hii,nathamini sana na ninaheshimu uamuzi wenu wa kuacha shughuli zenu ili kuja kujumuika nami”alisema Mbunge huyo.

 Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Mbogwe Nicodemus Maganga na kummwagia sifa tele kuwa ni kiongozi makini asiyetumbishwa na jambo lolote na kuwaomba wanambogwe kuendelea kumwamini kwa kuwa Chama Wilaya na Mkoa kinamwamini na kwamba kwa sasa aachwe afanye kazi kwa kuwa Uchaguzi bado.

“Mbunge Maganga ni kiongozi makini asiyetumbishwa na jambo lolote nawaomba wanambogwe waendelee kumwamini kwa kuwa Chama Wilaya na Mkoa kinamwamini na kwa sasa Mbunge Maganga aachwe afanye kazi kwa kuwa muda wa Uchaguzi haujafika si busara kuendelea kufanya mambo ya Siasa kwa kipindi hiki”alisema RC Shigela.

Akiongea na wananchi na Viongozi mbalimbali waliofika katika Sherehe hizo  Naibu Waziri Mkuu Dotto Mashaka aliwahakikishia wananchi wa Jimbo la Mbogwe kuwa Chama na Serikali kinamuamini na kumuelewa Mbunge huyo kwa namna anavyoisimamia Serikali na kukitetea Chama cha Mapinduzi.

“Mbunge Maganga ni mtu mwema,anajitoa kwa kila hali ni mtetezi wa wanyonge hasa wanambogwe na hata watanzania wote katika masuala ya Kitaifa”alisema Dkt Biteko.

 

 

Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi