Top News

 

   DED  MBOGWE: Jengo la Halmashauri kukamilika Agosti 2024.


Pichani ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Bi Saada Mwaruka 

Picha na Maktaba


pichani ni sehemu ya mbele ya Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe ambalo ambalo ujenzi wake unatarajia kukamilika Agosti 30.2024.

NA ANTHONY SOLLO MBOGWE.

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Bi Saada Mwaruka amesema,ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe utakamilika Agosti 30 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake,Mkurugenzi huyo amesema ujenzi wa Miradi hiyo uligubikwa na changamoto mbalimbali ikiwemo Jiografia ya Halmashauri hiyo,uchache wa Wahandisi pamoja na uhaba wa vyombo vya usafiri.

“katika Halmashauri yetu tuna changamoto nyingi ikiwemo Jiografia ya Halmashauri yetu,uchache wa Wahandisi pamoja na uhaba wa vyombo vya usafiri,utakuta Mradi unasimamiwa pembezoni mwa Halmashauri na usafiri katika Idara hautosherezi jambo ambalo linawafanya wataalamu wetu kushindwa kufika (Site) kwa wakati”alisema Mwaruka.

Changamoto katika Miradi hiyo ziliibuliwa Marchi 25 mwaka huu baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mbogwe akiongozana na Kamati ya Siasa pamoja na wajumbe wa Sekretarieti ya Chama hicho kutembelea Miradi inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali katika Halmashauri hiyo kupitia fedha zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

Hata hivyo baada ya kubainika kwa changamoto hizo wajumbe wa Kamati ya Siasa pamoja na Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi waligomea taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa jingo la Halmashauri hiyo na kumuagiza Mkurugenzi huyo kuandaa taarifa inayoakisi thamani ya Fedha.

April 9  mwaka 2024,waandishi wa Habari walifika katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ili kupata ufafanuzi kuhusiana na changamoto iliyopelekea kukwama kwa utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa jengo nla Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe ambapo Mkurugenzi huyo alisema tayari Serikali imesimamia kwa karibu changamoto hizo na sasa wamekubaliana kuendelea na shughuli za ujenzi wa jingo hilo na kwamba Mradi huo utakamilika Agosti 30 mwaka 2024.

“Serikali kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita imesimamia kwa karibu Mgogoro uliokuwepo baina ya Mkandarasi,Mhandisi Mshauri na Halmashauri na sasa pande zote tumekubaliana kuendelea na shughuli za ujenzi wa jengo hilo na kwamba Mradi huo utakamilika Agosti 30 mwaka 2024”alisema Bi Saada Mwaruka.

Aidha akitolea ufafanuzi kuhusu maelekezo yaliyotolewa na wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya waliofanya ziara mwezi Marchi mwaka huu,kuhusu ubora wa Miradi inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo Mkurugenzi huyo anasema,amepokea ushauri na mapendekezo hayo na Ofisi yake inayafanyia kazi.

“tumepokea ushauri mapendekezo pamoja  maelekezo yaliyotolewa na wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya walioongozwa na Mwenyekiti wetu wa Wilaya Ofisi yangu inayafanyia kazi na ninawahakikishia kazi zitafanyika kwa kiwango na ubora’alisema Mwaruka.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni C F Builders Limited inayotekeleza Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Eng Fred Chacha ameishukuru Serikali kwa kuingilia kati na kufanikisha kutatua changamoto zilizopelekea kukwama kwa ujenzi wa Mradi huo.

“Naishukuru Serikali kwa kuingilia kati na kufanikisha kutatua changamoto zilizopelekea kukwama kwa ujenzi wa Mradi huu, nimefarijika sana kwa kuwa kwa sasa Halmashauri imetuhakikishia kuwa watatulipa malipo yetu kwa wakati kutokana na hatua ambazo tutakuwa tunakwenda nazo katika kuhakikisha kazi hii inafanyika”alisema Eng Chacha.

Hata hivyo akibainisha changamoto zilizopelekea kukwama kwa utekelezaji wa Mradi huo Mkurugenzi wa Kampuni C F Builders Limited Eng Fred Chacha alisema Mifumo ya malipo pia ilichangia kwa kiasi kikubwa kwa kushindwa kushusha fedha kwa wakati na kupelekea kuwepo kwa Mgogoro baina yao na wadau wengine wakiwemo Mafundi na vibarua.

Mkurugenzi wa Kampuni ya CF Builders Limited ameahidi kuwa ataikamilisha kazi hii kwa viwango na kwa wakati kutokana na makubaliano ya Vikao vilivyopelekea maridhiano ya kuuhuisha Mkataba na kwamba kazi hiyo itakamilika kwa wakati na kwa ubora.

Kuhusu Ajira,Eng Chacha amewaomba wana Mbogwe kujitokeza kwa wingi kuja kuomba Ajira zitakazotangazwa katika Mradi huo kwa kuwa hizo ni fursa zinazowalenga moja kwa moja.

“niwaombe wana Mbogwe hasa Vijana kujitokeza kwa wingi kuja kuomba Ajira zitakazotangazwa katika Mradi huu hizi ni fursa zinazowalenga wao moja kwa moja,si busara kuleta wafanyakazi kutoka nje ya Mbogwe,lakini pia ni gharama kubwa hivyo niwakaribishe waje tufanye kazi hii kwa kushirikiana”alisema Eng Chacha.

Kampuni ya CF Builders Limited Eng imejizolea umaarufu katika utekelezaji wa Miradi mikubwa ya ujenzi ikishirikiana na Taasisi za Serikali ambapo Kampuni hiyo imejenga majengo mbalimbali ikiwemo Chuo cha Ufundi (VETA Shinyanga),Chuo cha Ufundi (VETA Chato),Chuo cha Ufundi(VETA Namtumbo),Chuo cha Ufundi(VETA Singida)Integrated Justice Centre ( IJC ) Buswelu Mwanza pamoja na Mahakama ya Ilemela.

Katika kuboresha na kusogeza huduma kwa wananchi,Serika Chuo cha Ufundi (VETA li ilitenga jumla ya Sh Bil. 3.9 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe ambapo ujenzi huo ulianza mwaka 2016 na ulitarajiwa kukamilika mwaka 2019 ambapo kutoka na changamoto zilizojitokeza kumepelekea kutokamilika kwa wakati Mradi huo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa Mbogwe.

Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi