Miaka Mitatu ya Rais Samia,Uongozi wa Mgodi wa Mwagala Gold Mine wamwaga mamilioni kwa jamii.
Pichani ni picha za Mitambo mbalimbali inayotumika katika shughuli za uchimbaji na uchakataji wa Madini katika Mgodi wa MWAGALA GOLD MINING (MGM)ulioko katika Kijiji cha Igurubi Kata ya Igurubi Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora
NA ANTHONY SOLLO IGUNGA.
MENEJA wa Mgodi wa MWAGALA GOLD MINING (MGM)ulioko katika Kijiji
cha Igurubi Kata ya Igurubi Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora
Steven Emmanuel Siame,ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweka
mazingira mazuri ya uwekezaji nchini.
Akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu miaka mitatu ya
Rais Samia Meneja wa Mgodi wa Mwagala Steven Emmanuel Siame amesema,katika
kipindi hiki cha miaka mitatu ya Rais Samia,wachimbaji wadogo wamenufaika na
namna Rais alivyofanikiwa kuifungua nchi hasa uwekezaji katika Sekta ya Madini
hususani kwa wachimbaji wadogo na wakati.
“katika kipindi hiki cha miaka mitatu ya Rais Samia,sisi
wachimbaji wadogo tumenufaika na namna Rais alivyofanikiwa kuifungua nchi hasa
kwa kukaribisha uwekezaji katika Sekta ya Madini hususani kwa wachimbaji wadogo
na wakati”anasema Siame.
Katika hatua nyingine Meneja wa Mgodi wa Mwagala Gold Mining
Steven Siame ameipongeza Serikali kwa kufuta Leseni za Utafiti zinazochukua
maeneo makubwa huku zikiwanyima wachimbaji wadogo fursa ya kuwekeza.
“Naipongeza Serikali kwa uamuzi wake wa kufuta Leseni za
Utafiti zilizokuwa zinazochukua maeneo makubwa jambo ambalo lilipelekea
kuwanyima wachimbaji wadogo fursa ya kuwekeza”anasema Siame.
Akizungumzia changamoto Meneja huyo pia ameiomba Serikali iwasaidie
wachimbaji wadogo ikiwa ni pamoja na kuwaongoza namna ya kupata Msaada wa
kufanya Utafiti wa miamba katika maeneo yao pamoja na kupata Mitaji yenye tija.
Ameiomba Serikali kupitia GST mbaye ni mlezi mama kwa
wachimbaji wadogo na wa Kati kuwapata fedha kwa wakati ikiwemo Mikopo yenye
masharti nafuu kutoka Taasisi za Fedha na kutoa wito kwa wawekezaji kutoka nje
kujitokeza kwa wingi ili kuungana na kuweka mazingira mazuri ya Kiufundi na
Teknolojia itakayoweza kuongeza Mapato ya Kampuni pamoja na Serikali kwa ujumla.
Chapisha Maoni