Mbunge Maganga Afanya Ziara Mgodi wa Nhungwiza.
Asikiliza kero za wananchi na kutoa Maelekezo ukarabati wa Shule ya Msingi Nhungwiza.
NA ANTHONYSOLLO MBOGWE.
MBUNGE wa Jimbo la Mbogwe Mkoani Geita Nicodemus Henry Maganga Octoba 9 2024 amefanya Ziara katika Mgodi mpya wa Nhungwiza na kusikiliza Kero za wananchi ambapo pamoja na mambo mengine Mbunge huyo alifanya ziara katika Shule ya Msingi Nhungwiza.
Akiwa katika viwanja hivyo Mbunge Maganga alitoa maelekezo kwa Uongozi wa Mgodi huo kufanya ukarabati wa Majengo ya Shule hiyo kwa kuyapaka rangi ili kuonyesha kiwango na hadhi ya Shule hiyo kwamba ndiyo iliyofanikisha kutoa Kiongozi mwakilishi wa wananchi.
Aidha katika ziara hiyo Mbunge Maganga aliongozana na Ofisa Madini Mhandisi Yohana Marwa ambaye baada ya kusikliza kero za wachimbaji wadogo wanaofanya shughuli zao katika Mgodi huo alitolea ufafanuzi wa mambo mbalimbali ikiwemo Sheria ya Madini inavyoelekeza kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo mwongozo wa Migao ya Asilimia za wamiliki wa Mashamba,pamoja na makundi mbalimbali.
Katika ziara hiyo iliibuka kero ya bei ya Madini ya Dhahabu ambapo wananchi walimuomba Mbunge kutoa Elimu kuhusu bei Elekezi ya kuuzia Madini yao ambapo Maganga alimkaribisha Ofisa MadiniMhandisi Yohana Marwa ambaye alitolea ufafanuziwa mambo mbalimbali ikiwemo ubora wa Madini yanayochimbwa katika Mgodi huo pamoja na ufafanuzi wa bei katika Soko la Dunia kwamba Serikali inasimamia kwa weledi na kuhakikisha wananchi wanapata stahiki zao kutokana na ubora wa Madini wanayopeleka Sokoni.
"Naomba wachimbaji mtambue kuwa bei ya Madini inategemea na ubora wa Madini mnayochimba katika Mgodi huu lakini pia bei katika Soko la Dunia inategemea na ubora wa Madini yanayopelekwa Sokoni yana ubora wa aina gani lakini niwahakikishie kwamba Serikali inasimamia kwa karibu changamoto zenu na kuhakikisha wachimbaji mnapata stahiki zenu kutokana na ubora wa Madini mnayopeleka Sokoni"alisema Mhandisi Marwa.
Kuhusu changamoto iliyotokea kipindi cha siku chache zilizopita Mhandisi Yohana Marwa alisema kuwa Serikali ilisikia kilio cha wanunuzi na kufanya Vikao katika ngazi mbalimbali ili kupata Suluhu ya Changamoto ya wanunuzi na kwamba kwa sasa hali imerejea na huduma zinaendelea katika masoko ya Madini nchini likiwemo Soko la Madini la Mkoa wa Kimadini wa Mbogwe.
Ofisa kutoka katika Ofisi ya Ofisa Madini Mkazi Mkoa wa Kimadini wa Mbogwe Mhandisi Yohana Marwa akitolea ufafanuzi juu ya hoja za wachimbaji katika mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Mbogwe uliofanyika katika Mgodi wa Nhungwiza Kata ya Bukandwe Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe 0ktoba 9 2024.
MBUNGE wa Jimbo la Mbogwe Mkoani Geita Nicodemus Henry Maganga akisikiliza kero katikaMkutano uliofanyika katika Mgodi wa Nhungwiza Kata ya Bukandwe Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe 0ktoba 9 2024.
Mbunge Maganga akitoa maelekezo baada ya kusikiliza Kero za wananchi katikaMkutano uliofanyika katika Mgodi wa Nhungwiza Kata ya Bukandwe Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe 0ktoba 9 2024.
Chapisha Maoni