Top News

Mbunge Tabasamu Aing'alisha Sengerema

 
 

SERIKALI INAENDELEA NA UTEKELEZAJI WA AHADI YA RAIS.

NA ANTHONY SOLLO BUNGENI DODOMA.

 SERIKALI imesema inaendelea kutekeleza Ahadi ya Rais wa Awamu ya Tano ya Ujenzi wa Km 15 Barabara katika Jimbo la Sengerema Mjini kwa kiwango cha Lami.

Akijibu swali NA 91 lililoulizwa na Mbunge wa Sengerema Hamis Mwagao Tabasamu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI amesema Serikali imeanza utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Awamu ya Tano YOUR APP HAS BEEN DISABLED ya ujenzi wa barabara kilomita 15 katika Mji wa Sengerema kwa kiwango cha Lami ambapo hadi kufikia sasa, Serikali imeshajenga jumla ya kilomita 1.69 zilizogharimu shilingi 974,936,260 zimekwishakamilika.

kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI ,Barabara zilizokamilika ni Kabita– Sengerema Sekondari kwa kiwango cha Lami yenye jumla ya urefu wa kilomita 0.97 na CCM - Bwawani na Pambalu yenye urefu wa kilomita 0.72.

"Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2024/2025, Serikali inajenga barabara ya Mapinda– Lubeho Hotel (kilomita 0.57) na Mabimbi - Beipoa (kilomita 0.43) kwa kiwango cha Lami kwa gharama ya shilingi 570,000,000.00, ambapo mchakato wa ununuzi unaendelea.

Aidha kwa sasa,Serikali inaendelea kufanya usanifu kwa barabara zilizosalia zenye urefu wa kilomita 12.31 kwa lengo la kupata gharama halisi za ujenzi na pindi fedha inapopatikana ujenzi uanze mara moja.

 
 
 
Mbunge wa Jimbo la Sengerema Hamis Mwagao Tabasamu akiuliza swali kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI kuhusu utekelezaji wa Ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kujenga barabara za kiwango cha Lami Kilomita 15 katika Jimbo hilo.
 
 

 

Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi