Top News

Mbunge Maganga Atikisa Bunge Ashauri kushughulikia changamoto Saba zinazowakabili wananchi.

MBUNGE wa Jimbo la Mbogwe Nicodemus Henry  Maganga ameishauri Serikali kushughulikia changamoto saba ambazo zinaikabili jamii ya watanzania.

Akichangia katika Mjadala wa Mpango wa Maendeleo wa 202/426 bungeni Dodima Novemba 7 mwaka huu Maganga ameainisha changamoto hizo na kupendekeza kuwa Serikali ihakikishe inasikiliza ushauri unaotolewa na Wabunge katika masuala mbalimbali.

kwa mujibu wa Mbunge Maganga,ni muda mrefu Serikali ikichelewesha ukamilishaji wa ujenzi wa maboma katika Halmashauri mbalimbali nchini ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe.

Licha ya ujenzi wa maboma hayo Maganga ameomba Serikali kuimarisha Mifumo mbalimbali ikiwa ni pamoja na NEST ili kuondoa ucheleweshaji wa Malipo ya Wakandarasi ambao wanaidai Serikali.

Mbunge huyo pia amezungumzua suala la Ajira kwa Vijana Mafao ya Wastaafu pamoja na upungufu wa Nyumba za Askari wa Jeshi la Polisi pamoja na kuimarisha Mfuko wa Maafa katika Halmashauri.


Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi