Top News

Mwamuzi Uingereza afungiwa kwa kuitukana Liverpool

Mwamuzi wa kati kwenye ligi kuu Uingereza anayefahamika kwa jina la David Coote amefungiwa kuwa mwamuzi wa ligi hiyo mara baada ya video iliyosambaa mtandaoni kusambaa ikimuonyesha akiitukana klabu ya Liverpool inayoshiriki ligi hiyo ambayo kwasasa imesimama ikipisha ratiba ya michezo ya timu za taifa.

David Coote amefungiwa kuwa mwamuzi wa ligi hiyo huku akipisha uchunguzi uendelee kufanyika na shirikisho linalosimamia waamuzi maarufu kama PGMOL ambapo watafanya uchunguzi kisha wakishajiridhisha ndiyo hukumu itatolewa atafungiwa kwa muda gani au kifungo chake kinamzuia kufanya nini na nini.Published from Blogger Prime Android App

Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi