Top News

VIDEO: Mbunge wa Geita, Mh. Constatine Kanyasu akichangia mjadala wa mpango wa taifa bungeni 5-Novemba-2024



Hivi ndivyo Mbunge Kanyasu alivyocharuka Bungeni Akiwatetea wakulima na wachimbaji wadogo akiitaka Serikali kufanya tafiti za Uwepo wa Madini.


Na Anthony Sollo Dodoma.


WAKATI wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muunganowa Tanzania wakiendelea na Mjadala kuhusu Mpango wa Taifa kwa mwaka 2025/26 Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Mh Costantine Kanyasu ameishauri Serikali kuboresha Sekta ya Kilimo cha kwa kuwa kuna fursa kubwa katika Sekta hiyo.


Akitoa Mapendekezojuu ya mpango wa Taifa amegusa Sekta mbalimbali ambapo

kwa upande wa Mifugo na uvuvi Kanyasu ameipongeza Serikali kwa kutenga fedha nyingi kwenye Vizimba huku pia akishauri Serikali kuwa makini hasa suala la kupunguza kodi kwa wafanyabiashara wanaoingiza Samaki kutoka nje.


kwa upande wa Madini Mbunge wa Jimbo la Geita Costantine Kanyasu ameipongeza Wizara ya Madini kwa utendaji mzuri ambapo Sekta ya Madini imechangia takribani asilimia 9 katika pato la Taifa ikichangia Dola bil 3.5.


Kuhusu Elimu Mbunge kanyasu amesema amegundua kuwepo kwa changamoto kubwa ya vipaumbele katika kipindi cha nyuma Serikali ilikuwa ikitoa kipaumbele kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya  Sayansi lakini kwa sasa wanafunzi hao wanakosa Chuo cha kwenda kusoma kutokana na ushindani.


Mbunge Kanyasu pia ameishauri Serikali iongeze Vyuo vya Madaktari katika katika kila ilipo Hospitali ya Kanda ili kutoa fursa ya kuendelea na Elimu kwa wanafunzi wa Taaluma hiyo.

Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi