Top News

Tanzania EU kushirikishana kufanya Utafiti wa Kina wa Madini pamoja na Mafunzo kwa vitendo kwa wataalam wa madini

Published from Blogger Prime Android App
Serikali yasema uongezaji thamani ni kipaumbele katika uvunaji Madini Mkakati

NA MWANDISHI WETU DAR ES SALAAM.

SERIKALI ya Tanzania imeaahidi kuendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) katika kufanya Utafiti wa kina utakaosaidia kupata taarifa sahihi za maeneo yanapopatikana Madini ili kuongeza uwekezaji katika uvunaji rasilimali Madini hususani madini mkakati kwa manufaa na maslahi ya Watanzania.
Published from Blogger Prime Android App
Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde ameyamesema hayo Desemba 11 Jijini Dar es Salaam alipokutana na ujumbe wa uwakilishi kutoka EU ukiongozwa na Bwana Hanspaul Stausboll ambaye ni Mkurugenzi wa Miradi ya EU Bara la Afrika na Kusini mwa Jangwa la Sahara. 
"Utafiti ni moyo wa Sekta ya Madini, ndiyo maana Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka kipaumbele katika utafiti wa kina wa madini kupitia mkakati kabambe ujulikanao kama Vision 2030 ambao umelenga kuongeza eneo la utafiti kutoka asilimia 16 ya sasa mpaka asilimia 50 ifikapo mwaka 2030.
Published from Blogger Prime Android App
Waziri Mavunde amesema,ni dhahiri kazi hiyo ni kubwa na Serikali haiwezi kuifanya peke yake pasipo kushirikishana na wadau.

"Taarifa njema ni kwamba tayari Serikali tumeshaanza kufanya kazi na EU katika utafiti kupitia Ubalozi wa Hispania nchini"anasema Waziri Mavunde.

Yapo maeneo ambayo tumeyatambua kwa ajili ya mradi wa kufanya utafiti wa kina wa kurusha ndege na tupo katika hatua za mwisho za kuanza kwa mradi huo wenye manufaa makubwa kwa Nchi yetu, aliongeza Waziri Mavunde.
Published from Blogger Prime Android App
Waziri Mavunde alibainisha kwamba mazungumzo hayo na ujumbe wa EU yamejikita katika kuimarisha mashirikiano kwenye uendelezaji sekta ya madini huku ikichagizwa na ukweli kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi chache ulimwenguni zilizobarikiwa madini mbalimbali yakiwemo ya kimkakati kama graphite ambayo ni kivutio kwa wawekezaji wengi kutokana na mwelekeo wa dunia katika kupunguza hewa ukaa ifikapo 2050 kwa matumizi ya nishati safi. 

"Eneo la pili tulilozungumza ni eneo la kuyaongezea thamani madini yetu ndani ya nchi badala ya kusafirisha yakiwa ghafi ambapo Nchi tunapoteza mapato, ajira na ustawi wa watanzania,haya ndio maagizo ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kutaka viwanda vya kuongeza thamani madini kujengwa nchini, hili pia limesisitizwa na Sera yetu ya Madini"alisisitiza Mhe. Mavunde.
Published from Blogger Prime Android App
Waziri wa Madini pia amesema, Miradi mbalimba inaendelea kufanyika nchini ikiwemo Mradi mkubwa unaojengwa Ngara, Mkoani Kagera wa Nikel ikihusisha Kampuni ya Tembo Nickel ambayo Serikali na mbia na Kupitia Mradi wa Nikeli ambapo Kampuni kubwa ya BHP anaingia kama mwekezaji,na kinakwenda kujengwa kiwanda kikubwa cha usafishaji wa madini ya metali pale Kahama kwenye eneo la Buzwagi Special Economic Zone ambacho kitakuwa na thamani ya zaidi ya Dola Milioni 500.
Hata hivyo,Waziri Mavunde alieleza fursa iliyopo katika Mradi wa Vijana na wanawake kwenye Sekta ya Madini ujulikanao kama Mining for Brighter Tommorow (MBT) na kutoa rai kwa EU kutoa ushirikiano zaidi katika Programu hiyo ili iweze kuleta Tija katika kufikia Uchumi wa kati wa juu na kuongeza pato la Mtanzania mara mbili ya ilivyo sasa kama malengo ya Dira ya Maendeleo ya 2050 ilivyoeleza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miradi wa EU kwa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara,Bw Hanspaul Stausboll amefurahishwa na hatua ambazo Serikali inazichukua katika uendelezaji wa sekta ya madini na kusisitiza kwamba EU ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika kufanikisha utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya kipaumbele ikiwemo Utafiti,ujenzi wa Miundombinu katika maeneo ya Migodi  na Mafunzo kwa Vitendo ili kuongeza ujuzi kwa Watanzania.
Published from Blogger Prime Android App

Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi