Top News

Makamu Mwenyekiti CCWT Abainisha chanzo cha Migogoro ya Ardhi Nchini.

Published from Blogger Prime Android App
NA ANTHONY SOLLO DODOMA.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT)Kusundwa Wamarwa amewataka Wafugaji kote Nchini kujiandaa na Mradi wa kuchanja Mifugo unaotarajia kuanza hivi karibuni kwa lengo la kuiongezea thamani Nyama kutoka Tanzania.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Jijini Dodoma, pamoja na mambo mengine Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji nchini amebainisha kuwa chanzo cha Migogoro ya Ardhi baina ya Makundi ya Wakulima Wafugaji na watumiaji wengine wa Ardhi ni kukosekana kwa mpango Madhubuti wa matumizi bora ya Ardhi kama Taifa.

Wamarwa amebainisha kuwa,kutokana na Utafiti uliofanywa na Taasisi hiyo,kwa sasa Nchi ya Tanzania imekuwa na Migogoro mikubwa ya Ardhi inayoyakumba makundi ya wafugaji,wakulima Pamoja na watumiaji wengine wa Ardhi.

“Kwa sasa Tanzania imekuwa na Migogoro mikubwa ya Ardhi inayoyakumba makundi ya wafugaji,wakulima Pamoja na watumiaji wengine wa Ardhi lakini chanzo kikubwa ni kukosekana kwa Utekelezaji wa Mpango wa Matumizi bora ya Ardhi Pamoja na Rushwa kutoka kwa baadhi ya Viongozi wa Serikali za Vijiji wakishirikiana na Watendaji wa Kata”anasema Wamarwa.
Makamu Mwenyekiti huyo anasema kuwa baadhi ya Wenyeviti wa Vijiji Pamoja na Watendaji wa Kata wamekuwa wakikutana na wafugaji wanaohamia katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kutafuta malisho na kumalizana nao kinyemela bila kufuata utaratibu wa kushirikisha Kamati za usimamizi wa maeneo ambazo ndizo zenye Mamlaka Kisheria ya kupokea Wafugaji.
Published from Blogger Prime Android App
Aidha Mkamu Mwenyekiti wa CCWT Taifa amelalamikia vitendo vya Viongozi hao kumalizana na Wafugaji bila kuita Mkutano Mkuu wa Kijiji ambao Kisheria ndiyo wenye Mamlaka ya kubariki ujio wa Wafugaji wanaoomba kuingia katika meeneo husika kwa lengo la kutafuta malisho.

Makamu Mwenyekiti huyo amesema kuwa katika nchi Hamsini Barani Afrika,Nchi yetu inashika nafasi ya pili kwa wingi wa Mifugo huku akifafanua kwamba kabla ya Sudani kugawanyika Tanzania ilikuwa inashika nafasi ya tatu kwa wingi wa Mifugo. 

Makamu Mwenyekiti aliyataja maeneo yenye Migogoro ya Ardhi na wingi wa Mifugo kuwa ni pamopja na Mikoa ya Morogoro,Ruvuma,Lindi,Mtwara na maeneo mengine machache.


Kuhusu wimbi la Wafugaji kuhamahama kwa Makundi ya Wafugaji,Wamarwa ameeleza kuwa ni kutokana na Makundi ya Wafugaji  kutafuta malisho ya Mifugo yao katika maeneo mbalimbali nchini baada ya wafugaji hao kukosa Malisho.


Hata hivyo Makamu Mwenyekiti huyo ametaja chanzo cha Wafugaji kuhamahama kuwa ni kutokana na kutokuwa na maeneo Maalumu yaliyotengwa na Serikali kwa ajili ya shughuli za Ufugaji 

Katika hatua nyingine Makamu Mwenyekiti huyo amewaonya Wenyeviti na Watendaji wa Vijiji kuacha kughushi nyaraka kusaidia wafugaji wanaohamia katika maeneo huku akiwaelekeza kufuata taratibu zilizowekwa na Serikali.

“Niwaombe sana Wenyeviti na Watendaji wa Vijiji kuacha mara moja kughushi nyaraka kusaidia wafugaji wanaohamia katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kutafuta malisho bali taratibu zilizowekwa na Serikali zifuatwe.

Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi